MSIMAMIZI wa Uchaguzi Jimbo la Madaba mkoani Ruvuma Shafi Kassim Mpenda ametoa rai kwa Makarani waongozaji na wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu kuwapa kipaumbele watu wenye makundi maalum siku ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28,2020.
Ametoa rai hiyo wakati anafungua mafunzo hayo katika ukumbi wa shule ya Madaba day iliyopo katika Kata Mkongotema Halmashauri ya Madaba .
Mpenda ametoa rai kwa Makarani waongozaji na wasimamizi kuwa waadilifu katika majukumu yao kwa kutoshabikia chama chochote wakiwepo kwenye kituo cha uchaguzi ili kulinda amani ya Tanzania.
‘’Wapo Mawakala wa vyama vya Siasa wapo kwaajili ya kusaka kura na kuna vyama 15 vilivyoshiriki uchaguzi kupigania au kulinda maslahi ya chama husika, isiwe sehemu ya kujenga urafiki na mawakala,wala mchakato wowote kwaajili ya mgombea wa chama chochote”.
Mpenda amewahakikishia Makarani waongozaji na Wasimamizi wa vituo usalama wawapo kazini siku ya uchaguzi na kuhakikisha wanawahudumia wananchi wote kwa usawa bila upendeleo.
Amewasisitiza Makarani waongozaji na wasimamizi wa vituo kuwa uchaguzi ni moja ya mambo manne nyeti kama vile Mitihani,Mwenge,Ziara za viongozi wa Serikali hivyo amesema kila mmoja ahakikishe anakuwa na nidhamu awapo katika kituo cha kupigia Kura.
Mwenyekiti wa Mafunzo hayo Denis Ngwahi amewaomba makarani wa uchaguzi kufanya kazi kwa umakini na kutofanya kazi kwa mazoea kwa sababu Tume ya uchaguzi wamewaamini.
Naye Msimamizi Mkuu Kata ya Lituta Agatha Ngunga kwa niaba ya wenzake amewaahidi kuwa uchaguzi utakuwa wa amani na watafuata maelekezo yote waliyopatiwa kwenye mafunzo hayo .
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
Oktoba 26,2020.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa