• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

MRADI wa Maji unaogharimu shilingi bilioni 2 utakavyomaliza kero ya Maji Madaba

Posted on: December 30th, 2020

SERIKALI ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli inatekeleza mradi mkubwa wa maji katika Mji wa Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 2.Meneja wa RUWASA wilaya ya Songea Mathias Pangras amesema mradi umekamilika kwa asilimia 75.

Amesema mradi umejengwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza walijenga chanzo na tank la lita laki mbili,na awamu ya pili wameongeza kujenga tank mbili na kazi ya usambazaji wa  maji kutoka kwenye tank kwenda kwa wananchi.

Mathias amezitaja gharama ya ujenzi ni zaidi ya shilingi bilioni mbili na milioni sabini na tisa, na mradi ukikamilika utamaliza tatizo la maji katika wilaya ya Madaba.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya songea Pololeti Mgema ametoa maagizo kwa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira kutoa elimu kwa wananchi wa Madaba kuhusu umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji.

Mgema ametoa maagizo hayo hivi karibuni wakati alipotembelea na kukagua chanzo cha maji cha Mgombesi kilichopo kilomita tano kutoka barabara kuu ya Songea - Njombe.

Mgema amesema wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za kiuchumi karibu na vyanzo ya maji wapewe elimu kuhusu umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji na athari zake kwa viumbe hai.

Mgema amesisitiza kwakusema wananchi wote wanaofanya shuguli za kiuchumi karibu na vyanzo vya maji ni marufuku kufanya kazi hizo kwalengo la kukabiliana na changamoto za ukosefu wa maji.

“ Maagizo yangu vyanzo vya maji vilindwe”,amesema Mgema.

Amesisitiza wataalam wa RUWASA kuongeza juhudi za kukamilisha ujenzi wa mradi huo ili uweze kutoa huduma kwa wananchi kama Serikali inavyopambana kuondoa tatizo la maji katika jamii.

Mgema amesema zaidi ya wakazi 30,000  wa  vijiji vya  kipingu,kifagulo,Mtepa na Lituta ndio wanufaika wakuu wa huduma hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa Kijiji cha Lituta na kipingu Esta Mlelwa na Godfrey Ngatunga ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha kipingu anakili kuwepo kwa tatizo la maji katika vijij hivyo lakini kwa sasa wanatoa shukrani kwa serikali kwa kuwaletea huduma ya maji

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa