WATAALAM wa Halmashauri ya Madaba wametambulisha mradi wa Boost katika Kata ya Mtyangimbole na Kata ya Gumbiro.
Akizungumza katika Mkutano wa wananchi Afisa Elimu Msingi na Awali Saada Chwaya amesema mradi wa Boost katika Kata ya Mtyangimbole upo katika Shule ya Msingi Ngembambili ambapo madarasa mawili yatajengwa na matundu ya vyoo matatu na fedha iliyotengwa ni shilingi Milioni 53,100,000/=.
Katika Shule ya Ngadinda iliyopo kata ya Gumbiro amesema yatajengwa Madarasa 2 na matundu ya vyoo 3 sawa na shilingi Milioni 53,100,000/= Fedha hizo zimekwisha ingia katika account ya Shule.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo katika Halmashauri hiyo Bashiru Mgwasa amezungumza katika mkutano huo uliojumisha kata 2 ametaja majukumu ya wananchi katika utekelezaji wa mradi ikiwa ni pamoja na kusafisha eneo la ujenzi,kuchimba msingi pamoja na kuchimba shimo la choo.
Diwawni wa Kata ya Mtyangimbole Erick Mkolwe amehamasisha wananchi hao kuhakikisha wanakuwa na umoja na mshikamano katika utekelezaji wa ujenzi wa miradi hiyo ili kuhakikisha wanamaliza kwa wakati ili Serikali iweze kuwaletea miradi mingine.
Naye Diwani wa Kata ya Gumbiro Gustaph Tindwa ametoa rai kwa wananchi wa Kata hiyo kuanza utekelezaji wa mradi huo mara moja ikiwa fedha zimekwishaingia katika accont ya Shule.
Kutoka ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Aprili 25,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa