MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amekabidhi msaada wa taulo za kike 2,502 zilizotolewa na Shirika la Social Action Trust Fund(SATF) kwa wanafunzi wa shule saba za msingi wilayani Nyasa.
Mndeme amemkabidhi taulo hizo na nguo za ndani 834 Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Isebala Chilumba katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mjini Songea.
Mndeme amezitaja shule ambazo zitakabidhiwa msaada huo kuwa ni zenye wanafunzi wa darasa la nne hadi la sita kutoka shule saba za msingi ambazo ni shule ya msingi, Kilosa, Likwilu, Muongozo,Ukuli,Kuhamba,Liparamba na Lumeme.
“Natoa wito kwa Halmashauri ya Nyasa,kuhakikisha inashirikiana na Shirika la SATF,kabla ya matumizi ya vifaa wanafunzi wapewe mafunzo kupitia klabu zao za afya’’,alisisitiza Mndeme.
Amesema kutolewa kwa vifaa hivyo ni juhudi za serikali za kuhakikisha kunakuwa na mazingira wezeshi ya kumhakikishia mtoto wa kike anapata elimu kwa kuhudhuria masomo na anadumu shuleni na kuhitimu masomo yake bila vikwazo.
Afisa Miradi wa SATF Makao makuu Edgar Kihwelo amesema shirika hilo linafanya kazi na Asasi za kiraia 19 katika mikoa 16 na wilaya 32 za Tanzania Bara.
Amesema tangu kuanzishwa kwa Shirika hilo watoto wanaishi katika mazingira magumu 193,000 wamesaidiwa na kuwawezesha kupata elimu na kaya zipatazo 900 zimejengewa uwezo kiuchumi.
Kulingana na Kihwelo,katika wilaya ya Nyasa kwenye mradi ulianzishwa mwaka 2019,Shirika limeweza kusaidia watoto wa shule za msingi 103 na watoto wa shule za sekondari sekondari 80.
Pia amesema wapo kwenye mchakato wa kuanzisha mradi wa tuwalinde katika Wilaya ya Madaba,Songea Vijijini na Nyasa ni mradi wa Mwaka mmoja na unamatokeo Mazuri katika kaya maskini.
Kihwelo amesema lengo la msaada huo ni kusaidia watotowanaoishi katika mazingira hatarishi wapatao 240 na kaya 160 na katika Wilaya 3 na mradi huo utabadilisha ushumi katika kaya na kuondoa utegemezi.
“Tunatoa Bima za afya iliyoboreshwa IHF katika kaya mnufaika mmoja anapata nafasi kupitia Bima na wanufaika tawano katika familia,tunashirikiana na Shirika la Good sumertantmission”.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo ,Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba amelishukuru Shirika la SATF kwa msaada huo ambao amesema utasaidia kumkomboa mtoto wa kike kielimu na kufikia ndoto zao.
Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Ruvuma Imanuel Kisongo amelipongeza Shirika la SATF kwa kuunga mkono jitihada za serikali za kumkomboa mtoto wa kike katika Mkoa wa Ruvuma.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Mdaba
Desemba 11,2020.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa