• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma azindua maadhimisho ya siku ya Mbolea Duniani

Posted on: October 11th, 2021

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amezindua maadhimisho ya siku ya mbolea duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Kabla ya kuzindua maonesho hayo RC Ibuge alikagua vibanda 41 vya washiriki wa maonesho ambayo yanafanyika kuanzia Oktoba 11 na kilele chake ni Oktoba 13.

Akizungumza na wananchi kwenye uzinduzi huo Mkuu  wa Mkoa wa Ruvuma,amesema Mkoa una chakula cha kutosha kwa muda mrefu ambapo katika msimu wa mwaka 2020/2021,Mkoa wa Ruvuma umezalisha tani 1,384,705 za mazao yote ya chakula na kuwa na ziada ya tani 894,960.

‘’Kwa zao la mahindi pekee uzalishaji ni tani 816,242 hivyo kuwa na ziada ya jumla ya tani 326,497 za mahindi’’,alisisitiza RC Ibuge.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,amesema uzalishaji huo unaambatana na matumizi ya pembejeo bora ikiwemo mbolea .

Ameyataja mahitaji ya mbolea katika Mkoa wa Ruvuma kuwa ni jumla ya tani 50,521 kwa msimu wa  kilimo wa mwaka 2020/2021 ambapo mbolea zilizoingia na kutumika ni tani 43,000 na kwamba katika msimu wa kilimo wa mwaka 2021/2022 Mkoa unatarajia kutumia mbolea tani 50,521 za aina zote za mbolea.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt.Stephano Ngailo  ameutaja mkakati mkuu wa serikali ni kuhakikisha kuwa mbolea inapatikana kwa wingi na bei nafuu kwa kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda vya mbolea hapa nchini.

Amesema serikali imeanza ujenzi wa kiwanda cha mbolea mkoani Dodoma ambacho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha mbolea za aina mbalimbali zaidi ya tani laki sita kwa mwaka.

Dkt.Ngailo amesema kiwanda hicho kinatarajia kuanza uzalishaji msimu wa mwaka 2022/2023,  ambacho amesema kitakuwa ni ukombozi mkubwa kwa wakulima hapa nchini wakiwemo wa Mkoa wa Ruvuma ambao wanaongoza kwa kuzalisha mazao ya chakula nchini.

Kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya mbolea duniani ni tumia mbolea bora, kwa tija na kilimo

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa