MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brig. Jen. Wilbert Ibuge amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ambaye kwa sasa ni Naibu katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara.
Ibuge baada ya kukabidhiwa ofisi hiyo amesema watumishi wa serikali na viongozi ni viungo vya kuwasaidia na kutetea maslahi ya wananchi wa Ruvuma na watanzania ili kuhakikisha Mkoa unakuwa salama na Tanzania kwa ujumla.
“Naombeni watumishi wenzangu tuwe wamoja kwaajili ya maslahi ya wanaruvuma ambao tumedhaminiwa kuwatumikia kwa lengo la maendeleo na wananchi waendelee kuiamini serikali yao waliyoiweka madarakani kwa kishindo kama hatuta pigania haki na usalama wao tutakuwa tumepotoka “.
Hata hivyo Ibuge ameendelea kuwasisitiza viongozi wote wa mkoa kuwa daraja ya kuwatumikia watanzania na amemshukuru aliyekuwa Mkuu wa Mkoa kwa kumpokea na kumwachia Mkoa na ameahidi kuutumikia Mkoa huo kwa ukamilifu.
Mndeme akimpongeza Ibuge kwa kuteuliwa na Rais Samia na amemkabidhi watumishi wa Ofisi hiyo na kuwaomba kumpa ushirikiano kwa kujituma.
“Nawaomba mfanye kazi kwa kujituma zaidi ya nilivyokuwepo mimi kila mtu kwa nafasi yake anapohitajika katika shuguli za utekelezaji wa maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma na kumpa ushirikiano Mkuu wa Mkoa“.
Mndeme akisoma taarifa ya makabidhiano amesema mafanikio yaliyopatikana nikutokana na ushirikiano aliopata kutoka kwa Wakuu wa Wilaya,Kamati ya ulinzi na usalama,Wakuu wa taasisi ,viongozi wa chama pamoja na wananchi kwa ujumla.
Amesema taarifa hiyo imezingatia Ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2015-2020 katika ngazi zote Serikali kuu na mamlaka katika serikali za mitaa imeainisha ,kuondoa umaskini,kupunguza tatizo la ajira kwa vijana,kuendeleza mapambano dhidi ya adui rushwa, ubadhilifu wa mali za umma na kudumisha amani na usalama wa raia pamoja na mali zao.
Mndeme amesema kwa kipindi cha mwaka 2015-2020 taarifa hiyo imezingatia utekelezaji wa dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2021-2025 mpango wa maendeleo ya Taifa ya miaka mitano,na mpango wa maendeleo wa miaka 5 wa kupunguza umaskini na kuongeza uchumi.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa habari Halmashauri ya Madaba
Mai 25,2021.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa