Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amezindua kumbukizi la miaka 115 ya mashujaa wa vita ya Majimaji na tamasha la utalii wa utamaduni lililofanyika kwenye viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Mahenge Songea
Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya Mashujaa ya majimaji vilivyopo Manispaa ya Songea amesema Februari 27, 1906 mashujaa wapatao 67 walinyongwa na wakoloni wa Kijerumani.
Ibuge amewaasa wananchi wa Mkoa huo kuendelea kuwaenzi mashujaa hao kwa kuwa walijenga msingi muhimu wa kupiga vita ukoloni na ubeberu dhidi ya nchi yetu ya Tanzania ikiwemo mikoa ya kusini.
”Kumbukizi ya Februari 27 kila mwaka inatoa fursa kwa Wananchi wa Tanzania na hususani Mkoa wa Ruvuma kuendeleza urithi wa utamaduni wa asili kwaajili ya vizazi vya sasa na vijavyo”.
Hata hivyo amesema kumbukizi hiyo inasaidia kuibua na kuendeleza fursa za utalii wa utamaduni wa Mkoa wa Ruvuma na Ukanda wa Kusini ili kuinua uchumi na kuboresha hali ya maisha ya wananchi.
“Serikali kwa lengo la kutambua na kuendeleza mchango wa Wajasiliamali na taasisi za serikali kwa kukuza uchumi kwa vitendo maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu Sera ya Tanzania ya Viwanda pamoja na kukuza utalii Ukanda wa Kusini”.
Mhifadhi wa Makumbusho ya Majimaji Batazar Nyamsya amesema vita hivyo vilitokea Julai 1905 mpaka 1907 Agosti na viongozi walioshiri katika vita hivyo walihukumiwa kunyongwa mpaka kufa Februari 27 1906.
Amesema wazo la maadhimisho hayo ilianzishwa na wazee wa Kingoni walitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa Martini Haule aliyekuwa ameteuliwa wakati huo na alichukua hatua ya dhati katika kushughulikia jambo hilo.
Nyamusya vifaa vya awali katika Makumbusho haya vilikusanywa na Mh.Dkt .Laulence Mtazama Gama padre chengula na baadhi ya wazee na kufufuliwa rasmi Julai 6,1980.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Hbari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Februari 23,2022
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa