MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele ameupongeza Mkoa wa Ruvuma kwa kuongoza kwa uzalishaji wa mazao ya nafaka nchini hivyo kuchangia pato la Mkoa kwa asilimia 75.
Meja Jenarali Mabele ametoa pongezi hizo wakati anazungumza na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas alipomtembelea ofisini kwake mjini Songea katika ziara ya kikazi mkoani humo.
“Niwapongeza Mkoa wa Ruvuma mimi nilikuwa Mbeya wakati mnakabidhiwa na Mheshimiwa Rais Tuzo ya mzalishaji wa kwanza wa mazao ya nafaka nchini,katika mikoa yote ninyi mlionekana mmefanya vizuri zaidi kwenye kilimo’’,allisisitiza.
Hata hivyo alisema anaamini Jeshi la Kujenga Taifa kambi ya Mlale wilayani Songea ,ni sehemu ya wazalishaji wa mazao ya nafaka hivyo katika tuzo iliyotolewa JKT Mlale pia wametoa mchango.
Amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa kutoa ushirikiano mkubwa katika kambi ya JKT Mlale ambapo amemuomba Mkuu huyo wa Mkoa kuendelea kuwatumia vijana wa JKT katika shughuli mbalimbali.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema katika msimu wa mwaka 2022/2023 Mkoa wa Ruvuma umezalishaji tani 1,598,163 za mazao ya chakula hali iliyosababisha Mkoa kuwa na ziada ya chakula tani 1,043,525.
Hata hivyo amesema kati ya tani hizo zao la mahindi pekee zimezalishwa tani 1,043,324 na kwamba wananchi 1,848,794 waliopo mkoani Ruvuma wanahitaji chakula tani 554,638 hivyo Mkoa kuwa na ziada kubwa ya chakula.Pichani katikati ni Mkuu wa Jeshi ;la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas mwenye suti ya bluu alipofika ofisini kwa Mkuu huyo wa Mkoa mjini Songea
Asilimia 87 ya wakazi wa Mkoa wa Ruvuma wanategemea kilimo.Kwa mwaka wanne mfululizo Mkoa wa Ruvuma unaongoza kwa uzalishaji wa mazao ya nafaka nchini.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa