Mkurugenzi wa Usimamizi wa Elimu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Vinsent Kayombo amezungumza na wataalam zaidi ya 280 kutoka mikoa ya Ruvuma,Njombe na Iringa wanaopata mafunzo ya Mradi wa Kuimarisha Ujifunzaji katika Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) Manispaa ya Iringa Iringa
Kayombo ametoa rai kwa wataalamu hao kuhakikisha wanakuwa na uelewa wa pamoja kupitia mafunzo hayo pamoja nakwenda kutekeleza mradi huo kwa ufanisi na kuendana na thamani ya fedha.
Kupitia mradi wa BOOST wenye lengo la kuboresha Elimu ya Awali na Msingi,serikali inatarajia kutumia shilingi trilioni 1.15 kutekeleza mradi huu kwa miaka mitano ambapo madarasa 12,000 na shule salama 6,000 zinatarajiwa kujengwa nchini .
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa