MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amezindua upandaji wa miti katika Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea.
Ibuge amesema tangu kuanza kwa mvua za masika Januari mwaka huu hadi sasa katika Mkoa imepandwa miti Zaidi ya milioni 2.4.
Ibuge ameyasema hayo wakati anazungumza baada ya kuzindua upandaji miti kwenye vyanzo vya maji kimkoa katika kijiji cha Mwande Kata ya Matetereka Halmashauri ya Madaba.
“Maelekezo niliyoyatoa siyo ya Mkuu wa Mkoa bali ni ya kitaifa kutoka kwa Mh. Rais na Makamu wa Rais ndiye anayesimamia mazingira ni mkakati lazima tuzingatie kwa kuhakikisha kila Halmashauri angalau kwa mwaka inapanda miti milioni 1.5’’.
Ibuge amesema miezi mitatu iliyopita ametembelea vyanzo vya maji amejionea uharibifu mkubwa wa ukataji wa miti hivyo ametoa rai kwa wananchi wote wa Mkoa kurejesha hali ya uoto wa asili ili kuwa na uhakika wa mvua na kulinda mazingira.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema katika uzinduzi huo amesema suala la upandaji wa miti limeshirikishwa katika Taasisi na Shule mbalimbali pamoja na wananchi wote wa Wilaya hiyo.
Afisa misitu Shamba la Miti la Wino Grory Kasmir katika zoezi la upandaji Miti amesema kufuatia maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wamefanya vikao na viongozi wa Wilaya ,RUWASA, pamoja na wananchi kuweka makubaliano ya kuhakikisha vyanzo vya maji wanaunda vikundi vya kulinda vyanzo vya Maji.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Februari 22,2022.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa