• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

MKOA wa Ruvuma waongoza tena uzalishaji chakula nchini

Posted on: November 5th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amewapongeza wakulima wa Mkoa wa Ruvuma kwa kuongoza tena nchini katika uzalishaji wa mazao ya chakula.

Mndeme amesema katika Mkoa wa Ruvuma  msimu wa mwaka 2019/2020 Mkoa wa Ruvuma umeongoza tena katika uzalishaji wa  mazao ya chakula na kuwa Mkoa wa kwanza kitaifa.

“Msimu wa 2020/2021,mahitaji ya chakula katika Mkoa wa Ruvuma ni tani 338,889 ikilinganishwa na tani 1,430,474 za mazao ya chakula zilizovunwa hadi mwezi Juni,2020 na hivyo kuwa na ziada ya tani 1,091,585’’,alisema Mndeme.

Amesema jumla ya hekta 474,901 zililimwa katika msimu wa mwaka 2019/2020  na kuzalisha tani 1,346,220 na kwamba katika msimu wa mwaka 2019/2020 Mkoa wa Ruvuma ulilima hekta 268,008 zilizotoa mavuno ya Tani 787,321 hii ni sawa na ongezeko la Tani 50,628 na kuongoza kitaifa katika uzalishaji wa mazao ya chakula.

Mndeme amesema Mafanikio hayo yaliyopatikana kwa miaka miwili mfululizo yametokana na uwepo wa nguvu kazi ya kutosha na utayari wa wananchi kushiriki katika shughuli za uzalishaji ambapo hadi sasa Mkoa una  chakula cha kutosha na ziada.

“Mkoa una jumla ya hekta 4,007,746 za ardhi zinazofaa kwa kilimo, katika kipindi cha Miaka mitano kuanzia mwaka 2015 - 2020 Mkoa umeweza kuzalisha tani 8,547,816 za mazao hadi kufikia mwaka 2020’’,alisisitiza.

Hata hivyo Mndeme ameyataja Mahitaji ya chakula katika Mkoa wa Ruvuma kwa mwaka 2020 ni tani 469,172 ikilinganishwa na uzalishaji wa mazao ya chakula ni tani 1,346,220 na hivyo Mkoa una ziada ya chakula tani 877,048.

Kulingana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,zao la Mahindi linaongoza kwa kulimwa kwenye maeneo mengi  hivyo kulifanya kuwa zao la chakula na biashara ambapo msimu wa kilimo wa mwaka 2019/20 Mkoa ulizalisha tani 787,321 katika hekta 268,008.

Amesema uzalishaji huo umechangiwa na matumizi ya zana bora za kilimo na matumizi ya pembejeo za Kilimo  kama mbolea na mbegu bora na kwamba matumizi ya mbolea yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka.

 Takwimu zinaonesha kuwa toka mwaka 2015 hadi kufikia 2020 mbolea iliyotumika katika Mkoa wa Ruvuma ni Jumla ya tani 167,758.5 ambapo Mkuu wa Mkoa amesema kiasi hicho cha mbolea kimepatikana kutokana na Serikali kuandaa mazingira mazuri ya uingizaji wa mbolea nchini.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Novemba 5,2020

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa