• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

MKOA wa Ruvuma wakusanya Bilioni 21 kutokana na Makaa ya Mawe

Posted on: November 16th, 2022

Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 21 kutokana na madini ya makaa ya mawe katika kipindi cha mwaka 2021/2022.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas wakati anatoa salama za Mkoa,kwenye mkutano wa wadau wa madini ya makaa ya mawe,uliofanyika kwenye ukumbi wa Parokia ya Bombambili mjini Songea.

Kanali Thomas amesema makusanyo hayo ni saw ana asilimia 179 ya lengo la mwaka,ambapo Mkoa ulipangiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 12.

“Katika kipindi cha hivi karibuni,makaa ya mawe yamekuwa yanahitajika sana ulimwenguni kama chanzo cha nishati na hivyo kuwa moja ya chanzo kikubwa cha mapato ya serikali’’,alisisitiza.

Hata hivyo amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2022/2023 Mkoa wa Ruvuma umepangiwa  kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 17 ambapo hadi kufikia Novemba 11,2022 tayari Mkoa umekusanya zaidi ya shilingi bilioni 15 sawa na asilimia 88.72.

Amesema hadi kufikia Juni 30,2023,Mkoa wa Ruvuma umelenga kukusanya mapato kutokana na madini ya makaa ya mawe yatakayofikia kati ya shilingi bilioni 35 hadi bilioni 40.

Naye Mgeni rasmi kwenye mkutano huo,Waziri wa Madini Dkt.Doto Biteko amewataka wawekezaji kwenye sekta ndogo ya makaa ya mawe kujenga mahusiano na jamii inayowazunguka.

“Wewe Mwekezaji uone aibu kuchimba makaa ya  mawe halafu watu Jirani ya mgodi wako  pale ni masikini wa kutupa,Watoto wao shuleni wanakaa chini,Mwekezaji unaingiza mapato ya bilioni mbili, lakini umeshindwa kujenga darasa la milioni 20 hiyo ni aibu’’,alisema Waziri Biteko.

Hata hivyo Waziri wa Madini amesema hivi sasa  ushirikishaji watanzania  katika sekta ya madini,serikali inafanya vizuri ambapo katika migodi yote nchini wafanyakazi waliopo,asilimia 97 ni  watanzania na katika migodi mingine asilimia 100 ni watanzania.

Amesisitiza kuwa katika hatua ya ushirikishwaji watanzania kwenye sekta ya madini,serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inastahili kupongezwa kwa sababu zamani sekta hiyo ilimezwa kwa asilimia kubwa na wageni na kwamba zaidi ya asilimia 70 ya  bajeti yote ya manunuzi katika migodi mikubwa inanunuliwa na watanzania.

Mkutano wa wadau wa makaa ya mawe umefanyika mkoani Ruvuma ukishirikisha watendaji wote wa Wizara ya Madini na mikoa inayozalisha madini hayo ikiwemo Ruvuma, Njombe,Songwe na Mbeya.

Mkoa wa Ruvuma una hazina ya makaa ya mawe zaidi ya tani milioni 227 ambayo yanatarajiwa kuchimbwa kwa miaka 300.

Imeandikwa na Albano Midelo

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma

Novemba 16,2022

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa