• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

MKOA wa Ruvuma unambolea za kutosha msimu mzima

Posted on: November 13th, 2020

MKURUGENZI Mtendaji  wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) Dkt.Stephan Ngailo amesema Mkoa wa Ruvuma una mbolea  ya kutosha ya aina zote itakayokidhi mahitaji ya wakulima katika msimu mzima.

Akizungumza wakati anakagua ghala la mbolea la SONAMCU mjini Songea,Dkt.Ngailo amesema amekagua maghala ya mbolea katika wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma na ameridhika kuwa mbolea ipo ya kutosha.

Ametoa rai kwa wakulima kuendelea kujiandaa kununua mbegu na kulima mashamba yao ambapo amesema mbolea zote zipo za kutosha  ikiwemo urea,DP,SA na NPK.

Amesema serikali imekusudia kuhakikisha kuwa mbolea za aina zote zinapatikana katika mikoa inayolima mazao ya chakula ukiwemo Mkoa wa Ruvuma, Njombe, Iringa, Songwe, Rukwa, Katavi,Kigoma na Tabora na kwamba serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa maeneo hayo yote yanapata mbolea ya kutosha.

“Katika nchi nzima tuna zaidi ya asilimia 60 ya mahitaji yote ya mbolea,tunatarajia kufikia kati ya mwezi Februari hadi Machi tutakuwa na asilimia 75 hadi 80 ya mahitaji yote ya mbolea nchini’’,amesisitiza Dkt.Ngailo.

Dkt.Ngailo amesema katika msimu huu,serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli imejipanga vizuri kuhakikisha wakulima wanapata mbolea za aina zote kwa wakati.

 Hata hivyo amesema katika tathmini iliyofanyika Oktoba mwaka huu,Tanzania ilikuwa na tani zaidi ya 65,000 za mbolea ya urea na kwa mbolea nyingine zote zilifikia tani  252,000 ambapo kiasi hicho cha mbolea kinaweza kufika hadi mwezi Februri 2021.

Ameongeza kuwa hivi sasa katika bandari ya Dar es salaam kuna meli imetia nanga inaendelea kupakua mbolea aina ya urea tani 18,000 na kuna tani nyingine za mbolea zinatarajiwa kuingizwa nchini wakati wowote.

Kwa upande wake Afisa Kilimo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Paulo Msemwa  amesema mahitaji ya mbolea katika Mkoa ni tani zaidi ya 50,000 ambapo hadi sasa zimeingia tani zaidi ya 13,000 .Amesema mbolea imesambazwa katika maeneo yote ya Mkoa hivyo  ametoa rai kwa wakulima kuandaa mapema pembejeo zote za kilimo  ili kuongeza uzalishaji.

Mkoa wa Ruvuma  katika misimu miwili mfululizo ya 2018/2019 na 2019/2020 umeongoza na kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika uzalishaji wa  mazao ya chakula,huku sababu kubwa ya kuongeza uzalishaji ni upatikanaji wa mbolea ya kutosha.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Novemba 13,2020

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa