• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

MKOA wa Ruvuma na Morogoro kuunganishwa na Barabara ya lami

Posted on: January 22nd, 2023

SERIKALI kupitia Wakala za Barabara TANROADS inatarajia kuanza mradi wa kuunganisha Mkoa wa Ruvuma na Mkoa wa Morogoro kwa barabara ya lami.

 Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa nchini ambayo tayari wilaya zake zote zimeunganishwa kwa lami na makao makuu ya Mkoa.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Ephatar Mlavi  amesema serikali inatarajia kutekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya Lumecha – Londo wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma hadi Kilosa – Kidatu mkoani Morogoro kwa kiwango cha lami.

Mhandisi Mlavi ameutaja mradi huo kuwa utahusisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, yenye urefu wa kilometa 512 ambao ukikamilika utaunganisha Mkoa wa Ruvuma na Morogoro kwa kiwango cha lami

“Mradi huu upo katika hatua ya kupitia zabuni za wakandarasi ambapo zilifunguliwa tarehe 26 Agosti 2022. Mradi huu utatekelezwa kwa kutumia mtindo wa Usanifu, Manunuzi, Ujenzi na Ufadhili  (Engineering, Procurement, Construction and Financing”,alisema Mhandisi Mlavi.

Hata Hivyo Meneja huyo wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma amesema utekelezaji wa mradi huo  unatarajia kuanza muda wowote baada ya hatua stahiki za manunuzi kukamilika.

Akizungumzia ujenzi wa Barabara ya Songea – Makambako kwa kiwango cha lami, Mhandisi Mlavi amesema serikali ya Awamu ya Sita inatarajia pia kutekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya lami sehemu ya Songea – Lutukira ikijumuisha na sehemu ya Mtwara korido yenye urefu wa kilometa 111.

Mhandisi Mlavi amesema katika utekelezaji wa mradi huo,Serikali tayari imeshaingia makubaliano na Mfadhili ambaye ni Benki ya Dunia na hivi sasa hatua za mradi huo zipo katika hatua za awali za manunuzi.

 Amebainisha Zaidi kuwa mradi huo utahusisha ujenzi wa kilometa 111 za lami ambazo zitajumuisha kilometa 14 za Songea bypass katika Manispaa ya Songea  na ujenzi wa barabara ya  Songea  hadi Lutukira Halmashauri ya Madaba yenye urefu wa kilometa 97 hivyo kuunganisha wilaya ya Songea mkoani Ruvuma na wilaya ya Njombe mkoani Njombe.

Hata hivyo amesema Mkoa wa Ruvuma kupitia Wilaya ya Nyasa tayari umeunganishwa na  Mkoa wa Njombe kupitia wilaya ya Ludewa kwa kutumia  daraja la mto Ruhuhu unaomwaga maji yake ziwa Nyasa.

Amesema mradi wa daraja la Ruhuhu ulianza  kutekelezwa Juni 2016 na kukamilika Oktoba 2021 kwa gharama ya Zaidi ya shilingi bilioni 8.9 ambao umeunganisha wilaya za Nyasa na Ludewa.

Katika mwaka wa fedha 2022/2023,TANROADS Mkoa wa Ruvuma iliomba bajeti ya Zaidi ya shilingi bilioni 41 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo. Hata hivyo, kiasi cha Zaidi ya Shilingi 28 ndiyo kimeidhinishwa kwenye bajeti ya 2022/2023.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Januari 23,2023

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa