• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

MKOA wa Ruvuma kuzalisha parachichi zaidi ya tani 37,000

Posted on: November 13th, 2022

MKOA wa Ruvuma unatarajia kuzalisha zao la parachichi  tani 37,500 ifikapo mwaka 2025.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kanali Laban Thomas amesema Mkoa  umelenga kuongeza uzalishaji wa zao hilo kama yalivyo mazao mengine ya biashara kwa lengo la kuwawezesha wananchi kukuza uchumi kwa miezi ya Februari na Mei kila mwaka.

RC Thomas amelitaja lengo kuwa ni kuongeza uzalishaji wa parachichi kutoka hekta 2,446 zinazozalisha tani 1,769 hivi sasa  na kufikia zaidi  tani 37,000 mwaka 2025 na kwamba uzalishaji huo utafikiwa kwa  kuweka mikakati itakayoongeza tija ya uzalishaji.

“Tija ya uzalishaji kwa eneo kwa sasa ipo chini ambapo uzalishaji kwa eneo la hekta moja ni tani 0.7228,miongoni mwa mikakati inayotekelezwa ili kuongeza uzalishaji wa zao la parachichi ni kuwezesha kuwaunganisha wakulima kupitia vikundi vya wakulima’’,alisema.

Mikakati mingine ameitaja kuwa ni kuwapatia wakulima mbegu za parachichi,kuwafundisha namna ya kuanzisha kitalu cha miche ya parachichi,kuwafundisha namna ya kubadi(grafiting),kuandaa shamba,kupanda na kuhudumia  miche ya parachichi.

Kwa upande wake Afisa Kilimo ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Onesmo Ngao,amesema katika msimu wa mwaka 2021/2022 ,wakulima wamehamasishwa kulima zao la parachichi ambalo hivi sasa lina soko kubwa ndani ya nje ya nchi hasa katika nchi ya China ambayo ina mahitaji makubwa ya zao hilo.

Akizungumza mjini Songea hivi karibuni Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Chen Mingjian alitoa rai kwa wakulima  wa Mkoa wa Ruvuma kuongeza uzalishaji wa zao la soya na parachichi kwa kuwa soko la mazao hayo nchini China ni kubwa.

Uzalishaji wa zao la parachichi mkoani Ruvuma unafanyika katika  wilaya za Songea,Mbinga na Nyasa.

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa