MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amewapongeza wadau wa Elimu kwa kiwango cha ufaulu wa matokeo ya kidato cha sita mwaka 2020 umefikia asilimia 98.68.
Akitoa taarifa hiyo wakati akifungua Kikao cha kamati cha Ushauri wa Mkoa amesema hali ya ufaulu katika mitihani ya Kitaifa ya Elimu ya Msingi na Sekondari mwaka 2020 matokeo yalikuwa asilimia 78.52,mwaka 2019 ufaulu ulikuwa asilimia 83.70.
“Naipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa kufaulisha kwa asilimia 85.51 na inatakiwa kuongeza juhudi ili kupandisha ufaulu zaidi kwani matokeo yanaonyesha wamefaulu kwa asilimia 66.68”.
Mndeme amesema katika kikao hicho miundombinu kwaajili ya Wanafunzi wa kidato kwanza 2021,Takwimu inaonyesha hadi kufikia Novemba 2020 kulikuwa na upungufu wa vyumba 43 kwaajili ya kidato cha kwanza.
“Nimetoa maelekezo kwa Halmashauri zote kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanaanza masomo Januari 2021,Tumejipanga vizuri hakuna mtoto atakaebaki nyumbani kwa kukosa nafasi na Mkoa wetu ni kati ya Mikoa 9 nchini ambayo wanafunzi wote waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza watapata nafasi.
Hata hivyo Mndeme amesema Mkoa unatekeleza Kampeni ya Magauni manne chini ya Kaulimbiu ya Niache Nisome,ambapo Serikali ya Mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu inapambana na kuhakikisha inaondoa vikwazo vinavyosababisha wanafunzi wa kike kushindwa kuhudhuria masomo.na kumaliza.
Amesema Vikwazo hivyo ni pamoja na Mimba za utotoni hali inayosababisha wanafunzi wakatishe masomo na kufifisha ndoto zao.
Mkuu wa Mkoa amesema katika kupambana na kikwazo Mkoa kupitia Halmashauri zake umejenga Shule za wasichana pamoja na kujenga Hostel kwa shule za kutwa ili kuwasaidia wanafunzi wa kike kuepuka vikwazo hivyo.
Amesema shule hizo zimejengwa katika Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma isipokuwa Halmashauri ya Madaba,Kamati ya Ushauri ya Mkoa imeona umuhimu wa kujenga Shule ya Sekondari ya Wasichana katika Halmashauri ya Madaba itakayo chukua wanafunzi kutoka maeneo yote ya Mkoa.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa habari Halmashauri ya Madaba
Januari 14,2021
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa