KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim amezindua chanzo cha maji kilichopo katika shamba la Miti wino.
Kaim mara baada ya kukagua ametoa pongezi za dhati kwa kazi nzuri zinazofanyika na Wakala wa Misitu Wino (TFS) ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi pamoja na kutoa miche kwa wananchi.
Kiongozi huyo amewapongeza wanakijiji cha Wino kwa kuhamasika kupanda miti katika maeneo mbalimbali na kutunza vyanzo vya maji.
“Hongereni wanakijiji kazi nzuri,sambamba na hilo Mh.Mkuu wa Wilaya tuendelee kuwaelimisha wananchi Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 zimebeba ujumbe unaohusiana na mabadiliko ya tabia ya nchi uhufadhi wa mazingira kupitia kauli mbiu isemayo tunza mazingira,okoa vyanzo vya maji kwa usalama wa viumbe hai na uchumi wa Taifa”
Meneja wa Shamba la Miti Wino Grory Kasmir akisoma taarifa kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 amesema shuguli za uhufadhi zinazotekelezwa ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa miti 2022/2023 hifadhi ya mistu imeweza kukuza miche milioni 7,683,861 na kuwagawia wananchi miche milioni 692,735.
Muhifadhi amesema sambamba na hilo wametoa elimu ya uhifadhi kwa jamii vyanzo vinavyotaka kutoweka ikiwa ni pamoja na mto mgombezi,kineneka,lupahila ,mnywamasi ,lutukila na chechengu pamoja na kuboreha madhari na kupanda miti maeneo yenye uoto wa nyasi .
Kutoa kitego cha Habari Halmashauri ya Madaba
Aprili 19,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa