KATIBU Tawala msaidizi Rasilimali watu wa Mkoa wa Ruvuma Bakari Ally Mketo amezindua maonyesho ya bidhaa za Kitanzania na kuwaasa akina mama kuwaheshimu waumezao.
Hayo amezungumza katika kongamano hilo na kutoa rai kwa wanawake wajasiliamali kulinda familia zao maana wanawake wengine mara baada ya kujipatia kipato kukosa uaminifu katika familia zao.
Akizungumza katika Kongamano hilo linaloendelea kufanyika katika Viwanja vya Bustani ya Manispaa ya Songea amesema Serikali inatambua mchango wa wanawake katika kukuza na kuimarisha Uchumi wa Nchi.
Mketo amesema maonyesho haya ni sehemu ya kutambua mchango wa wanawake katika biashara na ujenzi wa uchumi wa Taifa na kuwapa nafasi wanawake wafanyabiashara,kuwajengea uwezo kupitia mafunzo ya usindikaji,kubadilishana taarifa za kibiashara,uwekezaji,kujifunza,kurasimisha biashara pamoja na kuunganishwa na Taasisi mbalimbaliza.
“Wakati natembelea mabanda ya maonyesho nimejionea ubora wa bidhaa na huduma nyingi ambazo wanawake kutoka Ruvuma na Mikoa mingine mnazalisha
Hata hivyo Mketo amesema amewasihi wanawake kuendelea kuzalisha bidhaa zenye viwango ili kukidhi mahitaji ya soko pamoja na ushindani unapoongezeza na thamani ya biashara inaongezeka kuliko kuuza mazao kama yalivyo.
Mketo ametoa wito kwa wanawake kuhakikisha wanaitumia TWCC kwani ni chama kikubwa ,ni mtandao wa wanawake ambao uponchi nzima ambao ni kiunganishi kati ya Serikali na Wanawake wafanyabiashara Tanzania.
Mwenyekiti wa Chama cha wanawake Mkoa wa Ruvuma Xsaveria Mlimira akisoma Lisala kwa mgeni rasmi ameeleza changamoto wanayopata ni pamoja na mikopo inayotolewa kwenye vikundi haikidhi mahitaji na kutofikia malengo ya Tanzania ya Viwanda.
Mlimira ameeleza mafanikio waliyopata wanawake ikiwemo kufungua ofisi ya Mkoa ambayo ipo katika eneo la Kanisa la Anglikani pamoja na kufanya kongamano kubwa la wajasiliamali la wanawake Mkoa wa Ruvuama lilifanyika Agasti 25,2020, na kupata elimu kutoka Sido,TBS, na Taasisi za kifedha.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa habari Madaba
Septemba 29,2021
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa