WAZIRI wa Maliasili na Utalii Damasi Ndumbaro amezindua Mkakati wa utekelezaji wa Sera ya Misitu na Utiaji sahihi kanuni za uendelezaji wa Nishati ya Mkaa Mbadala.
Uzinduzi huo umefanyika katika Viwanja vya Majimaji Manispaa ya Songea katika Tamasha la Majimaji Selebuka na kauli mbiu imekuwa Misitu ni uchumi tumelithishwa tuwalithishe.
Amesema Misitu inamuhimu katika maisha ya mwanadamu inasaidia kutuletea mvua,na nyuki ikiwemo katika tamasha hilo umefanyika uzinduzi wa Nyuki Duniani na kuzinduliwa na Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda .
“Misitu ni chanzo cha nishati wengi tunatumia kuni kwenye kupika na mkaa unaotokana na misitu, ipo mikaa ya aina nyingi lakini wataalamu wametuambia kuna mkaa mbadala unaotengenezwa kupitia mazao ya misitu na kilimo ni muhimu katika nuchumi wanchi na kutoa ajira”.
Hata hivyo Ndumbaro amesema Mkaa huo ulikuwa hautendewi haki wataalamu baada ya kufanya utafiti wamegundua mkaa huo mbadala kuuzwa mpaka nchi za nje na kupata faida kubwa.
Ndumbaro akizungumzia mkakati wa sera ya misitu,kuhakikisha watanzania wanatumia mkaa mbadala ili kuweza kuokoa Misiti na kutunza mazingira na kujipatia kipato.
“Mkaa huo mbadala unatokana na mabaki ya miti,pumba za mpunga,malanda ya mbao,mabua ya mahindi na takataka hata sasa kunawafanyabiashara 19 wameanzisha viwanda vya kutengenezea Mkaa nchini na baada ya kusainikanuni hizo watasafirisha mkaa wao nchi za nje na kuchangia pato la taifa, sekta ya misitu inaingiza asilimia 3.5 na mkaa na kuni huingiza 1.5 baada ya kuzindua mkakati huo tunatarajia kuingiza 2.5 mkaa na kuni “.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii Dr. Ezekiel Mwakalukwa amesema utekelezaji wa Taifa wa sera ya misitu wa mwaka 1998 na mkakati wa miaka 10 kuanzia 2021 mpaka 2031,na kuongozwa na sera ya Taifa ya mwaka 1998 inamiaka 23 sasa tangia imeanza.
Mwakalukwa amesema utekelezaji wa sera hiyo umekuwa umekuwa ukitekelezwa kuanzia mwaka 2001 mpaka 2010 na mpango ulipomalizika ilikosa mwongozo wa kuongoza utekelezaji wa malengo ya sera ya Taifa ya Misitu.
“Kutokana na hatua hiyo Wizara ya Maliasili na Utalii iliunda kikosi kazi kwaajili ya kufanya tathimini ya kina ya sera ya Taifa ya mwaka 1998 kama malengo yaliyopo katika Sera hiyo yanatosha na kufikia uhifadhi endelevu katika Sekta ya Misitu nchini”.
Mkurugenzi amesema baada ya kupitia sera hiyo ilionekana kuwa bado inaweza kutumika na kuongoza Sekta ya misitiu mwaka 2020 Wizara ya Maliasili iliunda kikosi kazi kingine na kuandaa rasimu ya mkakati huo na kupiwa na wadau mbalimbali kwa kutoa maoni na katika warsha mbalimbali na kamati ya mazingira
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
Julai 30,2021
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa