SERIKALI ya Awamu ya sita imeleta fedha kiasi cha shilingi Milioni 360,000,000 kwaajili ya ukarabati wa Madarasa 24 Halmashauri ya Madaba.
Fedha hizo zimepelekwa katika shule za Msingi ya Matetereka,Ifinga,Wino na Luhimba ikiwa kila shule imepewa Milioni 90 kwaajili ya ukarabati wa madarasa 6.
Kamati ya Fedha Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wametembelea shule ya Msingi Wino ambapo ukarabati wa madarasa hayo umefikia asilimia 90 na baadhi ya madarasa yameanza kutumika.
Mtendaji wa Kata ya Wino Paskina Mhagama katika ziara hiyo amewashukuru viongozi kwa kupeleka fedha na kubadilisha muonekano wa Shule hiyo ikiwa wanafunzi wanapenda kusoma katika shule hiyo.
“Tunamshukuru Rais Samia na Mbunge wa Jimbo la Madaba kwa kutuletea fedha zimebadilisha muonekano wa shule”.
Hata hivyo Mtendaji ameomba kwa awamu nyingine kwa viongozi kutoa fedha kwaajili ya ukarabati wa madarasa yaliyobaki ikiwa watoto wanakataa kusomea katika madarasa ambayo hayajakarabatiwa.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halamshauri ya Madaba
Januari 23,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa