HALMASHAURI ya Madaba inatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Nguluma unagharimu kiasi cha Shilingi milioni 40.
Akitoa taarifa hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas alipotembelea Shule hiyo amesema Halmashauri ilipokea shilingi milioni 40 mnamo octoba 1,2022 kutoka Serikali kuu.
“Ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa umefikia hatua ya ukalimishaji pamoja na viti na meza 100,ujenzi ulianza rasmi oktoba 28,2022 na hadi sasa umefikia hatua ya ukamilishaji”.
Mkurugenzi amesema mradi huo wa vyumba viwili vya madarasa utasaidia kuleta manufaa makubwa kwa jamii na Taifa pamoja na kupata madarasa bora kwaajili ya kufundishia na kujifunzia na kupunguza changamoto ya ukosefu wa vyumba januari 2023.
Amesema upatikanaji wa samani kwaajili ya matumizi ya wanafunzi wawapo darasani utasaidia wanafunzi kupata kujisomea kwa bidii ikiwem na miundombinu bora kuwavutia wanafunzi kuhudhuria masomo.
“Wananchi wanapata matumaini kwa Serikali yao kwa vile wanaona inavyowahudumia kwa miundombinu bora”.
Hata hivyo amesema madarasa hayo yatasaidia na kuwezesha wanafunzi watakaoanza kidato cha kwanza Januari 2023 kupata nafasi wote kutoka katika Shule mbalimbali nchini.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Habari Halmashauri ya Madaba
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa