SERIKALI ya awamu ya sita imesikia kilio cha wananchi wa Halmashauri ya Madaba cha kufuata huduma ya malipo ya kodi zaidi ya kilomita 120.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Ruvuma Nikodemas Mwakilembe amesema kwa mda mrefu wafanya biashara wamepata changamoto kufuata huduma Mjini Songea ikiwa leo wamefungua ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) katika Halmashauri hiyo.
Ufunguzi wa ofisi umefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkurugenzi nakuambatana na hafla fupi,ikiwa ofisi za Mamlaka ya Mapato katika Halmashauri hiyo zitapatikana katika jengo la Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri.
“Ndugu wafanyabiashara wa Halmashauri ya Madaba leo tumekutana kwaajili ya ufunguzi wa Ofisi ya Mapato kutokana na mahitaji ya mda mrefu,Serikali ya Awamu ya Sita imesikia kilio chenu mkitembea umbali wa kilomita zaidi ya 120 mpaka Songea kutafuta huduma”.
Mwakilembe amemshukuru Mkurugenzi kwa kuwapokea na kuwapatia Ofisi ambazo zitasaidia wananchi na wafanyabiashara wa Madaba kwa urahisi na kuepuka changamoto ya kufuata huduma Songea.
Kwa upande wake aliyekaimu nafasi ya Mkurugenzi Sajidu Idrisa Mohamed ambaye ni Mkuu wa Idara ya Kilimo Joseph Mrimi katika uzinduzi huo amesema Ofisi ya Mkurugenzi ni miongoni mwa taasisi ya Serikali ambayo inatoa huduma kwa wananchi.
“Uwepo wa Ofisi ya TRA sisi kwetu Halmashauriri ya Madaba tutashirikiana katika kutoa huduma ikiwa ofisi ya Mkurugenzi tunatoa Lesen ya Biashara hivyo tutakuwa bega kwa bega kuwafikia wananchi”.
Makamu Mwenye kiti wa Wafanya biashara Mkoa wa Ruvuma Alhaji Issa Athumani katika uzinduzi huo ameipongeza Serikali ya awamu ya Sita kwa kuanzisha ofisi katika Halmashauri ya Madaba na kuwapunguzia umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.
“Niseme tu hii ni fursa kwasababu maafisa kuanzia sasa watakuwepo hapa na shughuli zenu wataziona ikiwa kulipo kodi ni haki hata vitabu vya Dini vimeelekeza”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Machi 20,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa