MKUU wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile amewahakikishia Madiwani wa Halmshauri ya Wilaya ya Madaba kumaliza mgogoro wa mpaka wa Songea Vijijini na Madaba kabla ya Mwaka 2023 kuisha.
Hayo amezungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya kwanza ya Mwaka 2023/2024 amesema Halmashuri ya Madaba inamwelekeo mzuri ikiwa hakuna jambo linalovunja moyo.
“ Mkuu wa Mkoa ameniagiza ofisi yake ikotayari kutoa ushirikiano wa asilimi zote mnapopata changamoto ikiwa jambo la mpaka wa Songea Vijijini na Madaba unaathiri mapato”.
Ndile amesema jambo hilo la mpaka linafanyiwa kazi kwa kina ili kuhakikisha mgogoro huo hauathiri kuingiza mapato kwa Halmashauri ya Madaba kwa kudai vijiji na vitongoji vipo upande wa Songea Vijijini.
“Nilimpa mrejesho Mkuu wa Mkoa na nilisisitiza Halmashauri ya Madaba ndio wenye haki ikiwa haina sababu ya kuegemea upande mmoja Wilaya ya Songea yote nasimamia mimi”.
Hata hivyo amesema Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Ruvuma amejiridhisha na wataalam kwa kuzingatia ramani na nyaraka zote.
Kutoka kitengo cha Mawasilino Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Novemba 11,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa