MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Jairy Khanga ametoa elimu ya chanjo ya homa kali ya mapafu (UVIKO 19) kwa waandishi wa habari na kuwaasa kutoa elimu sahihi kwa wananchi.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa aesema kuwa, ugonjwa huo huambukiza kwa njia ya majimaji mepesi ambayo hutoka katika mfumo wa kupumua, kinywa na macho.
Dr.Khanga akielezea afua sita za kujikinga na ugonjwa huo ni pamoja na kukaa umbali wa mita moja kwasababu hicho kirusi ni kizito hivyo hakiwezi kuruka kwa umbali mrefu,kutumia maji tililika kwa kunawa mikono kwa sabuni, kuvaa barakoa, kutumia vipukusi mikono, kupata chanjo, kufanya mazoezi na kupata rishe bora.
Hivyo ameendelea kuwakumbusha wanahabari na wananchi kwa ujumla kuzingatia afua hizo. Aidha, amewapongeza wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wanavyokuchukua tahadhari tangu UVIKO 19 ufike nchini machi 16,2020. Ameeleza kuwa, hata magonjwa ya kuharisha yamepungua kwa kuzingatia afua ya kunawa mikono mara kwa mara na sabuni.
Vilevile, Mganga Mkuu ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuleta Chanjo zaidi ya milioni 1 na Mkoa wa Ruvuma zimeletwa chanjo elfu 30 kwa ajili ya kinga dhidi ya UVIKO 19.
“Namshukuru Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa kuzindua chanjo Agosti 4, 2021 na chanjo hizo zinapatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya ambapo tulianza na vituo 23 lakini kwa sasa vituo vimeongezeka kwa kadri wananchi wanavyohitaji na tunatoa kwa njia ya mkoba kwa wananchi walikuokusanyika pamoja”.
Vilevile amesema kuwa, baada ya tatizo hili kuanza miaka mingi iliyopita Wanasayansi Duniani walijikita zaidi kutafuta Chanjoa ya UVIKO 19 mpaka kufikia sasa wamepata chanjo 312, lakini Shirika la Afya Duniani (WHO) limethibitisha chanjo 8.
Dr Khanga amesema vigezo vilivyo tumika kuthibitisha Chanjo hiyo vipo viwili ufanisi wa chanjo,kuangalia kama ni salama kwa matumizi ya binadamu kwa kutumia maabara zilizo bobea Duniani na kugundua zinafaa na kuongeza kinga dhidi ya UVIKO 19.
“Nyote mnafahamu Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliunda Timu ya Wataalamu Wabobezi katika chanjo nane ambazo zimethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na kwa Taasisi ya mamlaka ya vifaa tiba na madawa (TMDA) kutumia vigezo vitatu ambavyo ni kuangalia kama chanjo inafanya kazi kwa ufanisi, usalama wa chanjo kwa matumizi ya binadamu na mazingira ya Tanzania.” Alisema Khanga.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amesema, timu hiyo ya wataalamu imejiridhisha kuwa chanjo hiyo inafanya kazi vizuri pia ni salama kwa matumizi ya Binadamu na ina ufanisi kwa mazingira ya kitanzania. Hivyo, wameshauri Serikali ya Tanzania kuridhia matumizi ya aina 5 za chanjo kati ya 8 zilizothibitishwa na Shirika La Afya Duniani kupitia TMDA.
Dkt. Khanga ameeleza faida za Chanjo hiyo kuwa ni kutoa kinga thabidi dhidi ya UVIKO 19, kuzuia vifo dhidi ya ugonjwa huo na inazuia kupata athari kali za ugonjwa wa UVIKO 19. Vil, amewafahamisha wanachi wa mkoa wa Ruvuma kuwa, chanjo hiyo itawawezesha kupunguza gharama za matibabu.
Dkt. Khanga amewahiza wananchi wa Mkoa wa Ruvuma ambao hawajapata chanjo, wajitokeze kwa wingi kupata chanjo na kuepuka elimu mbaya zinazotolewa kwenye mitandao.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma
Agosti 8,2021.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa