• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

MFUMO wa stakabadhi ghalani wawaingizia wakulima Ruvuma zaidi ya bilioni 28

Posted on: April 14th, 2021

MFUMO wa stakabadhi mazao ghalani katika Mkoa wa Ruvuma umewawezesha wakulima kupata fedha zaidi ya shilingi bilioni 28.

Akizungumza wakati anafungua mkutano wa wadau wa mazao ya ufuta,soya na mbaazi kwenye ukumbi wa Songea Club,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme  amesema kiasi hicho cha fedha kimepatikana  katika msimu wa masoko wa mwaka 2020/2021.

Ameyataja mazao yaliuzwa katika mfumo wa stakabadhi ghalani kupitia minada mbalimbali iliyofanyika katika wilaya za Songea,Tunduru na Namtumbo kuwa ni  ufuta,soya na mbaazi.

Kwa mujibu wa Mndeme,zao la ufuta kilo 12,234,737 zilizouzwa na kuwaingizia wakulima zaidi ya shilingi bilioni 25,soya kilo 1,499,077 ziliuzwa na kuwaingizia wakulima zaidi ya shilingi bilioni moja na zao la mbaazi kilo 4,260,77 ziliuzwa na kuwaingizia wakulima zaidi ya sh.bilioni 2.585.

“Mfumo wa stakabadhi mazao ghalani umeonesha mafanikio makubwa katika Mkoa wetu,hivyo leo tunafanya tathmini ya msimu wa masoko uliopita 2020/2021 na kuratibu maandalizi ya msimu wa masoko wa 2021/2022 ambapo ununuzi unatarajia kuanza Mei 2021’’,alisema Mndeme.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amesema  mfumo huo umeziwezesha Halmashauri kukusanya ushuru kwa lengo la kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo kupitia zao la ufuta pekee zilikusanywa zaidi ya sh.milioni 954 za ushuru kwenye Halmashauri.

Mafanikio mengine ya mfumo huo ameyataja kuwa ni kufufuliwa kwa vyama vingi vya ushirika,kuongeza ajira na kwamba mfumo umerahisisha ukusanyaji wa kodi kwa ajili ya mapato ya serikali kuu kupitia TRA.

Awali akitoa taarifa ya mazao ya ufuta,soya na mbaazi kwenye mkutano huo,Mrajisi Msaidizi wa Vyama Vya Ushirika Mkoani Ruvuma Bumi Masuba ameutaja uendeshaji wa masoko ya mazao hayo,ulifanyika kupitia vyama vya msingi 44 mkoani Ruvuma na kuleta mafanikio makubwa.

Ameyataja maandalizi ya masoko katika mkoa wa Ruvuma msimu wa 20201/2022 kuwa yanaendelea kufanyika kwa mfumo wa stakabadhi za ghalani kupitia vyama vya ushirika.

“Makadirio ya uzalishaji wa mazao hayo katika msimu huu ni ufuta tani 15,437,soya tani 7,844 na mbaazi tani 2,889’’,alisema Masuba.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Aprili 13,2021

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa