WADAU mbalimbali Halmashauri ya Madaba wamejitokeza kutoa Zawadi kwa Wanafunzi Siku ya Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika
Meneja wa Shamba la Miti Wini Grory Kassmir akizungumza katika maadhimisho hayo amesema kwa kushirikiana na Jamii wamemuunga Mkono Mwenyekiti wa Halmashauri na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushiriki siku hiyo na kutoa Zawadi kwa Watoto.
“Kama Wakala wa Shamba la Miti Tanzania kwa upande wa Shamba la Miti Wino tumeleta Sabuni,taulo za kike,Sukari kilo 50,Daftari,Kalamu za Wino na Penceli.
Kassmiri amewaasa watoto wajifunze kusema hapana pamoja na kujiepusha na mazingira hatarishi ikiwa wazazi waache kutuma watoto usiku.
“Tuwe kama wazazi wa zamani ukimuona mtoto mwambie ondoka uende nyumbani lakini watoto wengi wanaharibika kwa kuzunguka usiku’’.
Mwenyekiti wa Halmashauri Teofanes Mlelwa amesema wapo na mashirika mbalimbali wamekuja na zawadi lakini kimsingi siyo zawadi ni haki yao hivyo wanakumbushwa kufanya hivyo mara nyingi.
Mlelwa amesisita na kuwaasa jamii kuwatunza watoto kama walivyoandika na kudai haki katika mabango yao, Kwa kupatiwa haki ya msingi ya Elimu,kupatiwa Afya ,haki ya kusikilizwa pamoja na malazi.
Hata hivyo katika maadhimisho hayo watoto wa shule ya Msingi Matetereka waamepewa zawadi mbalimbali ikiwemo taulo za kike,madaftari,peni,kalamu,mafuta ya kupaka,sukari na sabuni.
Amesema vifaa hivyo vimetolewa na wadau mbalimbali ikiwemo ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Madaba,Ofisi Shamba la Miti Wino(TFS),NMB Madaba,Mkinga Foundation Pamoja na Kikundi cha Bodaboda konabar.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Juni 16,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa