HALMASHAURI YA Madaba imezindua Chanjo ya COVID 19 (UVICO 19) itakayotolewa katika vituo viwili ikiwemo Kituo cha Afya Madaba na Dispensali ya Lilondo.
Mbunge wa Jimbo la Madaba Mh. Joseph Mhagama akizindua Chanjo hiyo ametoa taarifa ya Ugonjwa huo na kuhusu hali ya maambukizi yanayosababishwa na Virusi vya Corona (UVICO 19) katika Halmashauri ya Madaba.
Mhagama amesema kulingana na hali ya maambukizi ya UVICO 19 Dunia na Nchi jirani na Taifa letu ikiwemo Halmashauri ya Madaba haipo salama,juhudi za kudhibiti kwa kuenea Ugonjwa huo katika Halmashauri zichukuliwe kwa uzito.
“Kama tulivyoagiza na Rais Samia Hassan Suluhu kuwa ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona (UVICO 19) wimbi la tatu upo chini Tanzania na Halmashauri ya Madaba ikiwa ni sehemu ya Tanzania tunawajibu wa kusimama kidete kuhakikisha Ugonjwa huo unadhibitiwa katika Halmashauri yetu”.
Mhagama amelezea ugonjwa huo huambukizwa na huenea kwa njia ya majimaji kutoka kwenye mdomo au pua na sehemu nyekundu ya jicho,na kuepuka kwa ugonjwa huo kwa kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vipukusi mikono(Sanitizer),kuvaa barakoa,kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.
Mratibu wa huduma za Chanjo Halmashauri ya Mdaba Ayubu Faki akielezea faida za Chanjo ya UVICO 19 amesema inatengeneza kinga mwilini,inalinda mwili dhidi ya maradhi yanayosababisha na ugonjwa wa UVICO 19,inaepusha watu kupata madhara ya magonjwa makubwa, kupunguza uwezekano wa kumwambukiza mtu mwingine na kupunguza gharama kwa mgonjwa na Serikali.
Faki amesema Chanjo hiyo kwa awamu hii wametoa kipaumbele kwa watu wanaoshi na magonjwa sugu,watumishi wa sekta ya afya na watu wazima kuanzia miaka 50 na kuendelea na awamu itakayofuataitakuwa na watumishi wamipakani,wanadiplomasia,watu wa umri wa miaka 18 na kuendelea vikosi vya ulinzi,watalii,na wahubiri wa kimataifa.
Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dr. Mussa Rashidi mara baada ya uzinduzi huo amewasisitiza wananchi wa Madaba kujitokeza kwa wingi kupata chanjo hiyo na kuepuka minong’ono na maneno yanayosambaa kwenye mitanda ya kijamii na amewahakikishi kuwa chanjo hiyo ni salama.
Mkuu wa idara ya maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mdaba mara baada ya kupata chanjo hiyo amesema chanjo hiyo ni hiari na nimuhimu na ameshauri wananchi kutokuogopa kwasababu chanjo hiyo ni salama na itasaidia kupunguza maambukizi ya Ugonjwa wa Corona.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Mdaba
Agasti 8,2021
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa