MBUNGE wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ametembelea Hospitali ya Wilaya iliyojengwa kwa zaidi ya shilingi Bilioni tatu na kuanza kutoa huduma.
Mhagama amesema katika kamati hiyo anasimamia Wizara tano hivyo bado amekuwa kinara katika kuhakikisha Jimbo la Madaba linasonga mbele katika utekelezaji wa ujenzi wa miradi mbalimbali ya Serikali ambayo inaletwa Madaba.
Mbunge amewashukuru Viongozi wa chama cha Mapinduzi kwa kuonyesha ushirikiano pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Madaba wanaoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Sajidu Idrisa Mohamed kwa ushirikiano wanaouonyesha katika utendaji kazi.
“Nimepewa jukumu kubwa la kusimamia uchaguzi wa Rais wa Bunge la Dunia kama Mwenyekiti nimeongoza Nchi zote 180 Dkt Tulia Akson ni Rais wa Mabunge Duniani tumefanya jambo kubwa kuleta heshima kwa Nchi hii”.amesema Mhagama.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Madaba Teofanes Mlelwa amempongeza Mbunge wa Jimbo la Madaba kwa kuhakikisha Madaba inakuwa na Hospitali ya Wilaya na vituo vya Afya vitatu.
“Mbunge tunakushuru kwa kuhakikisha hata Zahanati zetu zinapata fedha na vituo vya Afya hizo ni juhudi zako pamoja na Rais tulikuwa hatuna ndoto ya kuwa na Hospitali ya Wilaya”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Februari 23,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa