Mbunge wa jimbo la Madaba Joseph Mhagama ametoa rai kwa wananchi wa Madaba wahakikishe wanajenga nyumba bora ili waweze kuwapangisha wageni mbalimbali wakiwemo watumishi wa umma.
Hayo amezungumza katika ziara yake ya siku ya nne katika akiwa ndani ya Jimbo lake na kata ya Lituta alipokagua nyumba ya mwalimu katika shule ya Msingi Kifaguro iliyojenjwa kwa shilingi milioni 50 na vyumba viwili vya madarasa ya awali vilivyojengwa kwa zaidi ya shilingi milioni 55 kupitia mradi wa LANES II.
Afisa Elimu Msingi vifaa na takwimu Raphael Kibirigi amemshukuru Rais Samia na Mbunge wa Jimbo la Madaba kwa kutoa fedha nyingi za ujenzi wa miundombinu ya elimu.
“Kama mnavyoona tumepata fedha na tumejenga madarasa ya kisasa watoto wanabembea na wanasoma katika mazingira mazuri”.
Imeanadaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasailaiano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Julai 18,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa