MBUNGE wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha analeta fedha za ujenzi wa miradi katika Kata ya Matetereka na Madaba kwa ujumla.
Akizungumza katika ziara yake ya siku saba ambapo ameanza na Kata ya Matetereka amesema kata hiyo imepata miradi mingi ikiwemo ujenzi wa kituo cha afya,ukarabati wa madarasa sita katika shule ya Msingi Matetereka,maji,ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari Matetereka, na barabara.
“Nimekuja na hawa viongozi wapate kuifahamu shule yetu na wapate kuona kazi ambazo tumefanya na tunazotakiwa kufanya”.
Mhagama amesema katika shule ya msingi matetereka bado kuna majengo yaliyosalia kwaajili ya ukarabatiwa pamoja na ujenzi wa bwalo la wanafunzi na jiko.
“Sisi mmetupa dhamana na tupo tayari kuendelea na kazi tukiongozwa na Mhe. Rais na bajeti ya mwaka huu tumetenga fedha na tutaendelea kutekeleza”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Julai 15,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa