JUMLA ya miradi 34 yenye thamani ya Sh. Bilioni 12,626,057,642.40 inatarajiwa kufikiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 iliyotekelezwa na Serikali na kusimamiwa na wananchi katika mkoa wa Ruvuma.
Mkuu wa mkoa huo Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amesema hayo leo(jana) wakati akiongea na waandishi wa Habari Ofisini kwake ambapo ameeleza kuwa,kati ya hiyo miradi miradi kumi yenye thamani bilioni 2,629,431,922.61 itazinduliwa.
Aidha ametaja,miradi minne yenye thamani ya Sh. Milioni 439,945,705.37 itafunguliwa,miradi minane yenye thamani ya Sh. Bilioni 8,192,394,296.40 itawekewa jiwe la msingi na miradi kumi na sita yenye thamani ya Sh. Bilioni 1,364,285,718.02 itatembelewa na kukaguliwa pamoja na kugawa vifaa mbalimbali.
Mkuu wa mkoa amesema, Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani Ruvuma utakimbizwa katika wilaya zote tano kuanzia kesho tarehe 2 Agosti hadi tarehe 6 kwa umbali wa km 1,055.1.
Ujumbe wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 umebeba ujumbe unaojikita katika umuhimu wa TEHAMA kwa maendeleo endelevu ya Taifa letu ambao unawakumbusha na kuwataka Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutumia maendeleo ya Tehama kwa usahihi.
Brigedia Jenerali Ibuge amesema, mkoa wa Ruvuma una shauku na ari kubwa ya kuupokea na kuukimbiza Mwenge wa Uhuru ili kutimza malengo yake.Pia,amewakumbusha wananchi wote kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Uvico 19 kwa kuvaa Barakoa muda wote wawapo kwenye mikusanyiko,kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni na kutumia vipukusa mikono mara kwa mara.
Brigedia Jenerali Ibuge amesema, katika maeneo yote ya mkesha wa Mwenge,zoezi la utoaji chanjo ya Uvico -19 kwa hiari litaendelea.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Septemba Mosi,2021
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa