Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsi na Wiki ya watoa msaada wa kisheria yamefungwa rasmi Mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeth Mgema akiwa mgeni rasmi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas katika uhitimishaji wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na wiki ya Msaada wa Kisheria yamefanyika katika Kata ya Ruvuma Manispaa ya Songea.
Mgema ameyataja madhara ya ukatili wa kijinsia kama vile ulemavu wa kudumu,kupoteza maisha tatizo la hakili,umasikini mkubwa unaotoka na kuto timiza wajibu wa kufanya kazi, na kuongezeka kwa watoto wa mtaani.
“Madhara hayo ya ukatili wa kijinsia yanasababisha madhara makubwa kwa maendeleo ya Taifa letu “.
Hata hivyo ametoa rai kwa kila mwananchi katika kijiji,Mtaa anaoishi kuwa salama na anapoona kuna swala la kikatili limetokea ahakikishe anatoa taarifa kwa vyombo vinavyotoa haki.
Afisa maendeleo wa Mkoa wa Ruvuma Xsaveria Mrimila akisoma taarifa ya hali ya ukatili wa kijinsia na Msaada wa Kisheria amesema Ukatili wa Kijinsia kwa watoto kwa lengo la kumdhuru au kumuumiza kisaikolojia Kimwili,kiafya,kingono na kiuchumi.
Mrimila amesema hali ya ukatili na matukio ya ukatili wa kijinsi kwa mwaka 2022 kwa mkoa wa Ruvuma yaliyobainika kwa kipindi cha miezi 6 katika Jeshi la polisi 442.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Desemba 10,2022.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa