Meneja wa Masile SACCOS Mbeya Rodina Mbwaga ametembele Mahanje SACCOS Madaba na timu yake kwa lengo la kujifunza katika maonesho ya Nane nane Mbeya.
Meneja wa Mahanje SACCOS Kassim Masengo akizungumza na watumishi wa SACCOS hiyo amewakaribisha kwaajili ya kujipatia elimu mbalimbali ikiwa Mahanje SACCOS ilianzishwa mwaka 1998 ikiwa na wananchama 68 na mtaji ulianzia shilingi elfu 68,000/=.
Masengo amesema hadi kufikia mwaka huu Juni ,2024 Mahanje SACCOS inawachama 1669 wameweza kukusanya akiba za wananchama zaidi ya shilingi milioni 400,amana za wananchama milioni 322.1,hisa za wananchama Milioni 140.5,akiba maalumu milioni 33.
“Kwa upande wa mikopo ni jumla ya shilingi milioni 776.1zimetolewa kwa wananchama na tumegawanya katika makundi,mkopo wa kilimo milioni 682, ujenzi milioni 32,biashara Milioni 32 ,ufugaji milioni 3.5,usafiri milioni 20.4 na elimu milioni 4.5”.
Aidha Masengo amesema Mahanje SACCOS inafanya kazi kwa ushirikiano Mkubwa na Halmashauri ya Wilaya ya Madaba akiwemo Afisa Ushirika wa halmashauri hiyo.
Kwa Upande wake Afisa Ushirika wa Halmashauri hiyo Sadam Fupi amesema kazi kubwa wanayofanya ni kuhakikisha wanalea SACCOS na kusimamia sheria za SACCOS na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara za kuangalia shughuli za chama.
“Chama cha Mahanje SACCOS kinatoa huduma kwa jamii na ni chama cha mda mrefu mambo yanaenda vizuri wananchama wanaongezeka na mikopo inalipika”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 5,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa