HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wamefanya kikao cha tathimini ya Mkataba wa Lishe cha robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Akitoa taarifa ya mafanikio ya utekelezaji wa mpango wa Lishe kwa kipindi cha robo ya pili Afisa Lishe Jovenary Ndelagi amesema wamefanikiwa kufanya tathimini na kutoa Elimu ya lishe na mtindo bora wa maisha kwa vijana rika balehe 365 katika shule 3 za Msingi na shule 2 za Sekondari.
Amesema wamefanikiwa kutoa Elimu ya lishe kwa wazee 137 katika maadhimisho ya wiki ya wazee Duniani Oktoba 1,Kata ya Lituta,pamoja na usambazaji wa matone ya vitamini A katika vituo 21 vya kutolea huduma ya afya kwa watoto wenye umri wa miezi 6 hadi 59.
Ndelagi amesema wamefanikiwa kutoa Elimu ya lishe kwa vikundi vya wanawake vitano juu ya ulaji na mtindo bora wa maisha katika vijiji 3 Madaba,Lituta na Kipingo.
“Tumefanikiwa kwa kipindi hicho kutoa elimu kwa wanaume 354 juu ya ushiriki wa wanaume katika matunzo ya wanawake wajawazito,wanaonyonyesha na watoto chini ya miaka mitano katika kijiji cha Ngadinda,Ifinga na Mbangamawe”
Hata hivyo amesema mikakati waliyojiwekea ili waweze kuboresha na kuifikia jamii kwa uwigo mpana zaidi ikiwa Halmashauri imetenga fedha kupitia mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ili kufanya mafunzo rejea ya kuwajengea uwezo wahudumu wa afya ngazi ya jamii.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Februari 5,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa