Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Olaph Pili amewataka wazazi kuwajibika vizuri katika kuhakikisha anapatikana mtoto kuanzia unapotafuta Ujauzito kwa makubaliano ya Baba na Mama.
Hayo amesema katika siku ya maadhimisho ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Kijiji cha Matetereka Kata ya Matetereka Halmashauri ya Madaba.
Amesema mwanzo mzuri hauanzii Mtoto anapoanza darasa la kwanza bali kuanzia ujauzito unapotafutwa na kulea kwa upendo.
“Mama anapopata Ujauzito asitelekezwe, asipotuzwa vizuri hawezi kupatikana mtoto aliye bora “
Pili amesema Mama akitunzwa akiwa mjamzito na akapata mahitaji yake ya msingi kula chakula bora,kwenda Kliniki kwa wakati,upendo wa baba na upendo wa jamii mtoto anazaliwa katika ubora.
“Tukumbuke mama akiwa mjamzito na akasemwa mtoto aliyetumboni anasikia kuwa mama yangu anasemwa,au akipigwa mtoto anasikia kuwa mama yangu anapigwa mtoto akizaliwa anakuwa ameathirika katika ubongo wake na kuwa mtoto wa ajabu katika familia na jamii”.
Hata hivyo Makamu Mwenyekiti amesema ili watoto bora wapatikane lazima wajawazito waheshimiwe na wapewe huduma zote za msingi.
Amesema watoto wanapozaliwa lazima wapelekwe kliniki na kupatiwa chakula bora ndipo watajengeka katika ubongo kwa kukua vizuri kuanzia miezi ya awali anavyoendelea kukua anakuwa katika hali njema.
Pili amesema watoto wanapoanza masomo yao kuanzia awali wazazi na walimu wahakikishe wanapata chakula wanapokuwa Shuleni itapelekea mwendelezo wa kufanya vizuri katika masomo yao.
Imeandalia na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Juni 16,2023
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa