WIZARA ya Katiba na Sheria inampango wa kujenga majengo ya Mahakama yanayoendana na hadhi iliyopo sasa na yale yaliyochakaa kufanyiwa ukarabati.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Joseph Pinda alipotembelea Mahakama ya Halmashauri ya Madaba.
“Mahakama zetu zina sura ya karne ya 21 tunakwenda kuleta Mahakama yenye hadhi nzuri lakini eneo la ujenzi liwe lenye hati na kiwanja kilicho pimwa”
Pinda ameelezea umuhimu wa huduma ya Mahakama kwa jamii ikiwemo kutokana na ongezeko la watu kuwa wengi na migogoro katika jamii kuongezeka siku hadi siku.
Hata hivyo Pinda amesema Mahakama nyingi zilijengwa Watanzania wakiwa milioni 9,kwa sasa tunakaridiliwa kuwa na Watanzania milioni 60 ambao kwa kipindi Mahakama ni Muhimu sana kwa jamii.
Pinda ametoa wito kwa Polisi kutokaa na kesi kwa mda mrefu mara baada ya upelelezi zipelekwe Mahakamani ili zipatiwe ufumbuzi na hukumu kwa watuhumiwa.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Habari Madaba
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa