SHULE ya Sekondari Magingo Kata ya Mkongotema Halmashauri ya Madaba wamefanya Mahafari ya 12 kwa wanafunzi wa kidato cha nne 2023.
Mgeni rasmi katika Mahafari hayo amekuwa Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama amewakilishwa na Mwenyekiti wa Halamshauri ya Madaba Teofanes Mlelwa amewapongeza Walimu kwa kuhakikisha wanafunzi hao wanahitimu Elimu ya Kidato cha nne na kuwazawadia Sukari kilo 25 itakayowasaidia kupata chai Shuleni hapo.
“Mimi nimewapa zawadi Walimu kwasababu natambua mchango wenu mzuri kwa wanafunzi hawa kwa kuishi nao hapa shuleni miaka mine na kuwapa Elimu ambayo itawasaidia kuingi kidato cha tano”.
Mkuu wa Shule hiyo Said Kunemka akisoma taarifa kwa Mgeni ramsi amesema Shule hiyo ilianzishwa rasmi mwaka mwaka 2009 na kusajiliwa rasmi kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo namba S .3979 na kupewa namba ya kituo cha mtihani S.4086 na Baraza la Mitihani.
Kunemka amesema Shule hiyo inajumla ya wanafunzi 292 ikiwemo wavulana 112 na wasichana 180 na inawalimu 16 wakiume 8 na wakike 8 pamoja na watumishi wasio walimu 7.
Hata hivyo amesema mafanikio ya ufaulu wa kidato cha nne wa shule hiyo kwa mda wa mika mitatu mfululizo Mwaka 2020 walifanya mtihani wanafunzi 31 na waliofaulu walikuwa 29,Mwaka 2021 walifanya mtihani wanafunzi 35 na walifaulu wanafunzi 32 pamoja na mwaka 2022 walifanya Mtihani wanafunzi 53 walifaulu 44.
“Mafanikio yanayotekelezwa kupitia Serikali ya awamu ya sita Shule hiyo imefikiwa na huduma ya Maji salama na wanafunzi kujipatia maji ya kutosha na kupata mda wa kujisomea,huduma ya umeme,huduma ya miundombinu kama vile maabara ,uwepo wa walimu wa kutosha,upatikanaji wa mashine ya kukoboa na kusaga”.
Amesema upatikanaji wa Televisheni ya Shule iliyonunuliwa na Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Kizito Mhagama pia ameishukuru Serikari inayoongozwa na Rais Samia.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Septemba 28,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa