WANAFUNZI 103 Katika Shule ya Sekondari ya Madaba day wanatarajia kuhitimu Kidato cha Nne mwaka 2023 katika Halmshauri ya Madaba.
Mkuu wa Shule Kelvin Kalesa akisoma taarifa katika Mahafari ya 22 yaliyofanyika Shuleni hapo amesema shule hiyo ni ya kutwa inawanafunzi 758 ikiwa kidato cha kwanza hadi kidato cha nne ni mchanganyiko wa wasichana na wavulana na kidato cha tano na sita wavulana pekee.
Kalesa amesema shule hiyo ilianza Mwaka 1996 ikijengwa kwa nguvu za wananchi mwaka 2002 Shule ilichukuliwa na Serikali na kupewa namba ya Usajili S.88 na kituo cha mtihani S.1199.
Amesema Shule hiyo inajumla ya Walimu 29 ikiwa wanaume 20 ni wanawake 9 na wafanyakazi wasio walimu 10.
Mkuu wa Shule amezitaja changamoto zilizopo shuleni hapo ikiwemo uhaba wa viti na meza kwaaajili ya Walimu na wanafunzi,Ukosefu wa Hosteli ya kidato cha kwanza hadi kidato cha nne.
“Mabweni yaliyopo yanatumiwa na kidato cha tano hadi cha sita yalijengwa na wananchi kwaajili ya kidato cha kwanza hadi nne”.
Amesema changamoto nyingine ni uchakavu wa madarasa yanayoonyesha kama shuleni hapo kuna shule mbili tofauti kuna madarasa ya kisasa na madarasa ya zamani.
Kwaupande wake Mgeni rasmi Mbunge waJimbo la Madaba Joseph Mhagama akiwakilishwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Olaph Pili amewaasa wanafunzi hao kuhakikisha wanasoma kwa mda mchache uliobaki na kuepuka kufeli na kupata Mimba za utotoni zitakazopelekea kuharibu ndoto kwa wanafunzi hao.
Pili ametoa rai kwa wazazi kuendelea kuchangia chakula cha wanafunzi Shuleni kwa hiyali ikiwa ni Sera ya Serikali na niwajibu wa kila mzazi kuchangia.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri amejibu lisala hiyo kwa niaba ya Mbunge amesema tatizo la uchakavu wa Madarasa na ukosefu wa hosteli wamelichukua watalifanyia kazi.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Septemba 30,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa