MADIWANI Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wamepewa mafunzo ya Maadili ya Uongozi katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya Pili 2023.
Akitoa mafunzo hayo afisa wa Maadaili kutoka ofisi ya viongozi wa maadili kanda ya Kusini Samweli Omary amesema Maadili ni kufanya kilicho sahihi iwe ni kwa kunena au kwa kutenda kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu zilizowekwa.
“Kama viongozi na watumishi wa umma mliopo katika ukumbi huu tunaendelea kuwahimiza kuwa waadilifu kwa kuzingatia sheria,kanuni na tarabitu na miongozo mbalimbali kila mmoja katika eneo lake”.
Hata hivyo Omary amesema kwa kila kiongozi ahakikishe anazingatia miongozo na kanuni za Nchi iliyowekwa na kiongozi akifanya tofauti na hapo atatafsiliwa amekiuka maadili.
Amesema Maadili yanasaidia kuchambua na kupambanua mambo mema na oevu mazuri na mabaya yanayokubalika na yasiyokubalika,yanayositirika na yasiyositirika na kuwezesha kufanya mambo sahihi kwa wakati wowote na mahali popote.
Mtu mwadilifu anapimwa kwa jinsi ambavyo anadumisha ushirikiano kwa watu au jamii inayomzunguka kwa kudumisha umoja na wale ambao anafanyanao kazi au jamii anayoiongoza.
“Madiwani,Wakuu wa Idara na watumishi wenzangu lazima tuonyeshe tunazingatia umuhimu wa maadili kwenye utumishi wa Umma tunaongozwa na Sheria kanuni taratibu na miongozo hata kwenye jamii ndio mana zipo sheria”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmshauri ya Wilaya ya Madaba
Januari 31,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa