Timu ya Madaktari bingwa 5 waliowasili Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Mkoani Ruvuma wanaendelea kutoa huduma katika Hospitali ya Wilaya.
Moja kati ya Madaktari Marti Burhani ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kupata matibabu ili kupunguza gharama kwa kufuata huduma katika Hospitali kubwa Nchini.
Hata hivyo amemshukuru Rais Samia kwa kuhakikisha analeta Madaktari bingwa ambao kupitia hao wamejifunza vitu vingi.
“Tunamshukuru Rais Samia kwa kutuletea Madaktari bingwa wametoa huduma kubwa katika magonjwa ya wanawake,watoto,na upasuaji”.
Hata hivyo amempongeza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo pamoja na Mganga mkuu wa Halmashauri kwa kuwapokea Madakri hao na kuwakarimu ikiwa wanafanya kazi kwa moyo.
“Licha ya kutoa huduma bora kwa wagonjwa sisi tumejifunza na wametusaidia kutujengea ujuzi zaidi”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Mei 9,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa