HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba imevuka lengo la kutenga kiasi cha shilingi elfu 1,000 hadi 4,684.54 za utekelezaji za mpango wa afua za lishe kwa kila mtoto chini ya miaka mitano.
Akitoa taarifa hiyo mratibu wa Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Madaba katika kikao cha tathimini ya utekelezaji wa mkataba wa Lishe kwa robo ya nne mwaka wa fedha 2023/2024.
“Asilimia za fedha zilizotumika za ndani kutekeleza afua za lishe katika halmashauri ni shilingi 9,205,126.6 sawa na asilimia 104.15”.
Hata hivyo waratibu wa lishe wamefanikiwa kutoa elimu kwa wazazi wenye watoto wenye umri wa mwezi 0 hadi miezi 23 lengo lilikuwa 786 na wamefanikiwa kutoa elimu kwa wazazi 786 sawa na asilimia 100.
Aidha amesema wamefanikiwa kutoa elimu ya ulaji unaofaa katika kijiji cha Ndelenyuma na Lilondo kwa wanufaika wa TASAF wakiwa wanawake 193 na wanaume 53.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 28,2024
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa