• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

MADABA yatumia milioni 196 kujenga mabweni mawili

Posted on: March 23rd, 2021

JUMLA ya shilingi milioni 196 zimetolewa na serikali kutekeleza  miradi ya ujenzi katika  shule ya Sekondari Mahanje iliyopo Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri hiyo Michael Hadu amesema kati ya fedha hizo shilingi milioni 150 zimetumika kwa kujenga mabweni mawili,milioni 40 zimejenga madarasa mawili na milioni 6.6 zimetumika kujenga matundu ya vyoo.

 Amesema mabweni hayo yana uwezo wa kulaza wanafunzi 160 kila moja hivyo kupunguza kero kwa wanafunzi wa kike ambao walikuwa wanasafiri kila siku kilometa 24 kwenda na kurudi kwenye makazi yao.

Hata hivyo  amesema Halmashauri  ya Madaba ina jumla ya shule nane za sekondari ikiwemo shule ya  sekondari Mahanje ambayo  imefanikiwa kujengewa mabweni mawili ikiwa na wanafunzi zaidi ya 526 wanaosoma kidato cha kwanza hadi cha nne.

“Tuliweka mikakati ya kuboresha miundombinu ya shule hiyo ikiwemo mabweni,maabara,madarasa,maktaba na vyoo  kwa kweli mabweni haya yamesaidia kupunguza mimba kwa wanafunzi na kuongeza ufaulu”,alisema Hadu.

Akizungumzia maendeleo ya taaluma katika Halmashauri hiyo,Hadu amesema kwa miaka miwili mfululizo 2019 na 2020,Halmashauri hiyo  imeshika nafazi ya kwanza kimkoa kati ya Halmashauri nane za Mkoa wa Ruvuma katika mtihani wa Taifa wa kidato cha nne.

 Kaimu Mkuu wa shule ya sekondari Mahanje Agastini Mikibalisi amesema ufaulu katika shule hiyo  umeongozeka na kuondoa alama ya sifuri ambapo mwaka 2018 shule hiyo ilishika nafasi ya 25 kati ya shule 75 za Mkoa wa Ruvuma,mwaka 2019 ilishika nafasi ya 35 kati ya shule 137 za Mkoa wa Ruvuma na  mwaka 2020 ilishika nafasi ya 24 kati ya shule 145 za Mkoa wa Ruvuma.

 Amesema mabweni hayo yameleta faida katika shule hiyo na kufikia idadi kubwa ya wanafunzi wanaohudhuria  masomo yao na kufanya vizuri katika mitihani yao.

Imeandikwa na Aneth ndonde

Afisa Habari halmashauri ya Madaba

Machi 23,2021

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa