WANANCHI wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wamefikiwa na Chanjo ya Surua na Rubbela 7215 ambapo lengo lilikuwa kuwafikia watu 6950.
Hayo amesema mratibu wa chanjo wa Halmashauri ya Madaba Claudius Makori kuwa ugonjwa wa Surua kwa watoto unaathali mbalimbali ikiwemo masikio kuto usaa na kusababisha kuto sikia,vidonda vya macho na kusababisha upofu, Nimonia,utapia mlo,kuvimba ubongo na kifo.
Makori amesema dalili za ugonjwa wa Surua kuwa na homa mafua na kikohozi,macho kuwa mekundu na kutoa maji pamoja na vipele vidogo hutokea kuanza katika paja la uso, nyuma ya masikio.
Hata hivyo amesema ugonjwa wa Rubbela husababishwa na Virusi vya Rubbela na kuenezwa kwa njia ya hewa,huwapata watoto wadogo hata kwa mama mjamzito.
“Ugonjwa huo ukimpata mama mjamzito unaleta athali kama vile mtoto wa jicho,Matatizo ya moyo,Kutosikia vizuri,mtindio wa ubongo na matatizo ya ukuaji wa mwili”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Februari 17,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa