HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba kupitia kitengo cha Lishe kwa mwaka wa fedha 2022/2023 wamefanikiwa kutoa Elimu ya lishe katika Kata na Vijiji .
Akitoa taarifa hiyo Afisa Lishe wa Halmashauri hiyo Joseph Peter katika Kikao cha Tathimini ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe, robo ya kwanza 2023/2024.
Peter amesema mafanikio hayo ni pamoja na kutoa Elimu ya Unyonyeshaji kwa wazazi wenye watoto chini ya miaka 5 wapatao 486 katika Zahanati ya Magingo,Hanga Ngadinda na Maweso na kutoa matibabu ya Utapiamlo kwa watoto 4.
Amesema wamefanikiwa kuwajengea uwezo waratibu wa Lishe ngazi ya Vituo wapatao 21 ya masuala mbalimbali,ukaguzi wa vyakula katika maduka ya vyakula 30 katika Kata ya Lituta na Mahanje.
Hata hivyo Afisa Lishe amesema changamoto zinazowakabili wananchi ikiwa msimu wa kilimo wazazi wengi kuhamia mashambani na kuacha kuzingatia malezi ya watoto pamoja na wajawazito kupelekea kuathiri afya zao.
Kutowafanyia mafunzo rejea kwa masuala ya Lishe kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii ambapo kupelekea kuathiri utoaji wa huduma sahihi za Lishe.
Peter ameelezea mikakati ya kutatua changamoto hizopamoja na kuendelea kutoa Elimu ya lishe na malezi na mafunzo kwa jamii ili kuhakikisha watoto na wajawazito wanakuwa na hali nzuri ya lishe.
“Halmashauri kutenga fedha kupitia mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ili kufanya mafunzo rejea kuwajengea uwezo wahudumu wa afya ngazi ya jamii”.
Amesema kuendelea kufanya maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ya kijiji, kuimarisha utoaji wa Elimu pamoja na Halmashauri kuunda klabu za Lishe kwa wanafunzi na kuhamasisha utekelezaji wa shughuli za lishe.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Oktoba 25,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa