Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed amewapongeza watumishi wa HALMASHAURI hiyo kwa ushirikiano na kuhakikisha wanafanya vizuri katika utekelezaji wa shughuli za Lishe kwa kipindi cha miaka miwili Kitaifa na Mkoa.
Mkurugenzi amesema hayo katika kikao cha lishe cha robo ya pili Oktoba hadi Disemba 2023/2024 mwaka 20221/2022 Madaba ilikuwa nafasi ya pili Kitaifa na mwaka 2022/2023 ilikuwa nafasi ya nne Kitaifa.
“Nawashukuru watumishi wenzangu kwa kufanya vizuri na kuhakikisha tunafanya vizuri kitaifa na Kimkoa Mungu awabariki sana”.
Naye Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Akitoa taarifa katika kikao hicho Jovenary Ntelagi amesema Halmashauri katika kupambana na lishe duni pamoja na utapiamlo wamefanya uchunguzi wa hali ya lishe kwa watoto chini ya miaka mitano.
“Tumehakikisha lishe bora inazingatiwa kwa makundi yote muhimu na kuepuka matatizo yanayotokana na lishe duni na kutoa unasihi wa lishe bora kwa kina mama wajawazito,wanaonyonyesha na wazazi/walezi wa watoto wenye umri chini ya miaka 5”
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Februari 23,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa