HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wamefanya kikao cha Liche cha maandalizi ya mpango wa bajeti ya afua za Lishe kwa mwaka wa Fedha 2024/2025.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed akifungua kikao hicho amesema bajeti hiyo itakayopangwa lazima isimamiwe katika utekelezaji wake ipasavyo.
“Nitoe wito katika idara ya Elimu Msingi na Sekondari kuhakikisha wanazingatia kila kilichowekwa katika bajeti “
Mkurugenzi amesema katika uandaaji wa bajeti hiyo wahakikishe wanazingatia vipaumbele vya msingi hasa katika shule ikiwemo kilimo cha bustani pamoja na ufugaji.
Hata hivyo amesema mwaka 2023/2024 Halmashauri imefanya vizuri katika utekelezaji wa bajeti ,hivyo ameagiza kuzingatia vigezo vyote vya miongozo ya bajeti ili kuhakikisha changamoto hazijitokezi.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Novemba 21,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa