HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wameadhimisha Miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika kwa kupanda Miti 500, Kufanya usafi na kuchangia damu salama katika Hospitali ya Wilaya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed akizungumza mara baada ya zoezi hilo amesema miti iliyopandwa ni ya kuzuia ukame ,Miti ya matunda pamoja na vivuli pia amewapongeza wananchi pamoja na Watumishi kwa kushiriki zoezi hilo.
“Wananchi wa Madaba mmekuwa wazalendo mmejitokeza kupanda miti katika eneo hili mmefanya kazi nzuri sana leo ni kumbukumbu kubwa kwenu”
Hata hivyo Mkurugenzi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha kwaajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.
“Tuendelee kumwombea Rais Samia katika kuadhimisha siku hii ambapo miaka 62 tangu tumepata Uhuru na mmejionea kazi nzuri inayofanyika katika Halmashauri yetu”.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Teofanes Mlelwa amewashukuru Wananchi waliojitokeza katika zoezi la upandaji wa Miti katika kuadhimisha Miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Disemba 9,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa