MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Ahmed Abbas Ahmed ameipongeza Halmashauri ya Madaba kwa kupata hati safi kwa miaka sita mfululizo tangu ilipoanzishwa.
Kanal ametoa pongezi hizo katika hotuba iliyosomwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Rehema Madenge katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani cha kujadili taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) juu ya Mamlaka ya Serikali za mitaa kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Hata hivyo Katika baraza hilo ametoa maelekezo ili halmashauri iendelee kupata hati safi kwa miaka mingine ijayo ihakikishe hoja zote zinafungwa,kuzuia kurudia hoja za aina ileile kila mwaka ,wakuu wa idara kushiriki ipasavyo kuandaa majibu ya hoja.
“Halmashauri ichukue hatua za kinidhamu kwa watumishi wanaozalisha hoja kwa uzezembe mkifinya watu watajua haina haja ya kuzalisha hoja zisizo na sababu”.
Aidha amesema kuhakikisha wananzuia matumizi ya fedha mbichi na kuzingatia kanuni,taratibu na sheria za fedha ili kuepuka kuwa na hoja ambazo zinazuilika.
“Hakikisheni mnawafuatilia wadaiwa sugu wote vikiwemo vikundi vya wanawake,vijana na wenyeulemavu,na kusimamia kwa ukamilifu CHF iliyoboreshwa ili kuhakikisha wananchi wengi wanajiunga na kupatiwa huduma za afya”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasailiano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Julai,12,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa