WATUMISHI wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wafanya mazoezi ya viungo kufuatia Mwenge wa Uhuru unaotarajia kuwasili Aprili 19,2023.
Mazoezi hayo yameongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Oraph Pili kuanzia ilipokuwa ofisi ya Halmashauri ya zamani hadi uwanja wa Shule ya Msingi Njegea ambapo Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukesha katika viwanja hivyo.
Hata hivyo mazoezi hayo yamejumisha watumishi pamoja na wananchi wa Halmashauri hiyo ili kuhakikisha wanaupokea Mwenge wa Uhuru kwa kishindo na wanaukimbiza ipasavyo na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa Fredrick Chaula ambaye ni Mtendaji Kata ya Wino ametoa rai kwa wananchi wote na watumishi kushiriki mazoezi ya viungo kila siku ya Jumamosi saa 12.00 asubuhi ili kuhakikisha wanajiandaa kimwili na kihakili katika kuupokea Mwenge wa Uhuru unaotarajia kuingia Mkoa wa Ruvuma Aprili 17,2023 kna kupokelewa katika Wilaya ya Tunduru.
“Wananchi na watumishi wenzangu kipekee naomba niwakaribishe katika zoezi la viungo kila Jumamosi saa 12.00 asubuhi ili tuulaki Mwenge wa Uhuru kwa ukakamavu”.
Kutoka Kiengo cha Mawsiliano Halmashauri ya Madaba
Machi 18,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 10
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: info@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa