• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

MAAGIZO 12 ya Kikao kazi cha Serikali mtandao kwa wakuu wa Taasisi Nchini

Posted on: February 15th, 2023

MAAZIMIO 12 YA KIKAO CHA TATU CHA SERIKALI MTANDAO KILICHOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA AICC JIJINI ARUSHA KUANZIA TAREHE 8/2/2023 HADI 10/2/2023

Maazimio hayo ndiyo maagizo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Jenista Mhagama kwa wakuu wa Taasisi na watumishi wa umma nchini  wakati anafunga kikao kazi hicho jijini Arusha.

1.Taasisi za Umma ziwajibike kutumia TEHAMA katika utoaji wa huduma kwa wananchi kwa njia ya kidijitali ili kuboresha utendaji kazi wa Taasisi

2.Taasisi za umma zihakikishe  zinaendesha shughuli za kawaida za Taasisi kidijitali kama vile uendeshaji wa vikao vya menejimenti,Bodi,Halmashauri na vikao vya mabaraza ya madiwani ili kupunguza matumizi ya karatasi.

3.Kila Taasisi ya umma ihakikishe tovuti ya Taasisi inakuwa na taarifa zilizouhisishwa na  zinazoendana na wakati muda wote pia tovuti hizo ziboreshwe ili kuendana na teknolojia ya kisasa.

4.Taasisi za umma zitoe kipaumbele katika masuala ya  utafiti na ubunifu kwenye eneo la TEHAMA ili kuibua mifumo ya TEHAMA itakayowezesha Taifa kuendana na kasi ya maendeleo ya viwanda ikiwemo kutenga rasilimali fedha kwa ajili ya  ubunifu.

5.EGA kwa kushirikiana na Taasisi za umma iendelee kujenga mifumo shirikishi na mifumo ya kisekta katika jitihada za kupunguza upungufu wa mifumo kwenye utumishi wa umma.

6.Wakuu wa Taasisi za umma wanalazimika kujiunga kwenye mfumo mkuu wa serikali wa kubadilishana taarifa ili  kuwezesha mifumo kubadilishana taarifa.

7.Taasisi za umma zinalazimika kuhifadhi mifumo yao kwenye vituo vya kuhifadhi data za serikali vilivyoidhinishwa na Mamlaka ya serikali Mtandao ili kupunguza gharama na kuongeza usalama.

Aidha usalama wa mifumo uliokwishajengwa uendelee kuimarishwa ikiwa ni Pamoja na kuwa na vituo vya kujikinga na majanga

8.Wakuu wa Taasisi za umma wasimamie kikamilifu utekelezaji wa sheria ya mtandao namba kumi ya mwaka 2019 na kanuni zake za mwaka 2020 hasa uanzishwaji wa Kamati za Uongozi wa TEHAMA na kusimamia utendaji kazi wa Kamati hizo

9.Serikali ianzishe utaratibu wa kuwafanyia upekuzi  Pamoja na matamko ya kiapo  watumishi wa TEHAMA kwa kuwa wanasimamia mifumo na data nyeti za serikali.

10.Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi iweke mkakati wa kuandaa wanafunzi wa  vyuo vya elimu ya Juu katika kufanya ubunifu  kwenye masuala ya serikali mtandao  na TEHAMA kwa ujumla.

11.Serikali iwekeze na kuanza kutengeneza vifaa vya TEHAMA hapa nchini

12.Mifumo ya TEHAMA ya serikali inayojengwa iwe endelevu ili  kuepuka kubadilisha mifumo mara kwa mara kwa kuwa hadi mfumo kuanza kutumika kunakuwa na uwekezaji mkubwa.

Watumishi wa umma 1600 kutoka mikoa yote nchini walishiriki kikao kazi hicho wakiwemo makatibu Tawala wa mikoa yote,wakuregenzi,wawakilishi kutoka Zanzibar ,wakuu wa Taasisi za serikali na watumishi wengine wa umma.

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa